DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: Rais Magufuli ataja mamilioni yaliyookolewa kwa Wanafunzi hewa
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa takriban shilingi bilioni 3.6 zimeokolewa kutokana na zoezi la kuwao...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa takriban shilingi bilioni 3.6 zimeokolewa kutokana na zoezi la kuwaondoa wanafunzi hewa kuanzia shule za msinngi hadi vyuo vikuu nchi nzima.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na namna ambavyo pesa za umma zinatumika kwa matumizi hewa kila mahali akitolea mfano wa wanafunzi hewa nchini ambao wamegundulika baada ya fedha za elimu bure kuanza kuingia mashuleni.

"Tumekuwa tukitoa shilingi 18.77 bilioni kila mwezi kwa ajili ya kutekeleza elimu bure lakini kumekuwa na wanafunzi hewa na shilingi bilioni 3.6 zimeshaokolewa kutokana na zoezi la uhakiki lililofanyika nchi nzima kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu” amesema Rais Magufuli.

Rais ametolea mifano ya wanafunzi hewa katika mikoa ya Mwanza na kusema kuwa kuna wilaya ina wanafunzi hewa 5,000, Arusha kuna wilaya ina wanafunzi hewa 9,000 na Dar es Salaam 7,000.

Sambamba na hayo Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini kufanya uhakiki upya wa vyuo vikuu nchini ili kubaini ubora na vigezo vya wanafunzi wanaostahili kujiunga navyo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. Lwekaza Mundara amesema kuwa hosteli hizo zinazojengwa kwa shilingi bilioni 10 kutoka serikalini, zikikamilika zitasaidia kubeba wanafunzi takriban 3,840.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top