Karibu Malingumu Blogspot, Leo katika label yetu ya afya tunakuletea baadhi ya mambo yaliyomo katika vipodozi . tafadhali soma na chukua hatua.
SEHEMU YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.
Hivyo hujumuisha :
-Vipodozi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)-Vipodozi vyenye viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)-Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha-Vipodozi ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi)-Vipodozi ambavyo maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza
Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.
1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:
Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine)Steroids (Mifano ni Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, na Dexamethasone)Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayoChloroformBithionolHexachloropheneMercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayoVinyl chlorideZirconium na kemikali zinazotokana nayoMethyelene chlorideHalogenated salicylanilides (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan na Tetrabromsalan)Chlorofluorocarbons (Kwenye pafyumu na deodorants)
1.2 JINSI YA KUJUA KAMA KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU
Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.
Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).
Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.
Mifano
Sabuni ya JARIBU ina kiambato MERCURY. Sabuni hii sio salama, haifai kwa matumizi na imepigwa marufuku.Losheni/krimu ya MEKAKO ina kiambato HYDROQUINONE. Losheni/krimu hizi sio salama, hazifai kwa matumizi na zimepigwa marufukuKrimu za FAIR & LOVELY SUPER CREAM, VISIBLE DIFFERENCE CREAM, SKIN SUCCESS FADE CREAM, DEMOVATE NA DIPROSON CREAM zina viambata Krimu hizi sio salama kutumika kama vipodozi na zimepigwa marufuku
SEHEMU YA PILI
2.0 MADHARA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA
Vipodozi visivyo salama vina madhara mengi sana kwa afya ya mtumiaji. Na kama mtumiaji ni mjamzito basi madhara hayo yanaweza kumpata na mtoto aliyepo tumboni.
Pia vipodozi hivi vina athari nyingi sana kiuchumi kwani vitapelekea mtu kutumia pesa tena kugharamia matibabu ya matatizo atakayopata. Madhara hayo ni pamoja na:
-Ugonjwa wa saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na kibofu cha mkojo-Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo-Magonjwa ya moyo na kutopumua vizuri-Kutokwa na chunusi kubwa kubwa-Ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele-Ngozi kuwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda kitachelewa kupona au hakitapona-Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi-Kichefuchefu, kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu-Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu (hasa kichwani)-Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na waliopo tumboni-Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi-Kuchubuka kwa ngozi-Ngozi kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali-Upofu, uziwi na upotevu wa fahamu wa mara kwa mara-Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
2.2 USHAURI
Kama tulivyoona hapo juu mengi ya madhara ya vipodozi visivyo salama ni makubwa na huhatarisha kabisa afya za watumiaji na watoto. Hivyo ni vyema kuvijua na kuviepuka kabisa ili usiweze kupata madhara.
Pili msaidie kumuelimisha ndugu, jamaa na rafiki nay eye ajue na asitumie kabisa vipodozi visivyo salama
Pia ukiona mtu au duka ambalo linauza vipodozi visivyo salama acha kununua vipodozi kutoka kwake na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa
Epuka kabisa vipodozi visivyo salama. Hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
SEHEMU YA TATU
3.0 ORODHA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA
Vifuatavyo ni vipodozi visivyo salama na vimepigwa marufuku kutumika. Epuka kabisa kutumia vipodozi hivi hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
3.1 Krimu, Losheni na Jeli zenye kiambato cha Hydroquinone
Mekako CreamRico Complexion CreamPrincess CreamButone CreamExtra Clair CreamMic CreamViva Super Lemon CreamUltra Skin Tone CreamFade-Out CreamPalmer’s Skin Success (Pack)Fair & White Active Lightening CreamFair & White Lightening CreamFair & White Strong Bleaching Treatment CreamFair & White Body Clearing MilkMaxi-Tone Fade CreamNadinola Fade CreamClear Essence Medicated Fade CreamPeau Claire Body LotionReine Clair Rico Super Body LotionImmediate Claire Maxi –Beauty LotionTura LotionLkb Medicated CreamCrusader Skin Toning CreamTura Bright & Even CreamClaire CreamMiki Beauty CreamPeau Claire Crème EclaircissanteSivoclair Lightening Body LotionExtra Clair Lightening Body LotionPrecieux Treatment Beauty LotionClear Essence Skin Beautifying MilkTura Skin Toning CreamMadonna Medicated Beauty CreamMrembo Medicated Beauty CreamShirley CreamKiss – Medicated Beauty CreamUno21 CreamPrincess Patra Luxury Complexion CreamEnvi Skin TonerZarina Medicated Skin LightenerAmbi Special ComplexionLolane CreamGlotone Complexion CreamNindola CreamTonight Night Beauty CreamFulani Cream EclaircissanteClere Lemon CreamClere Extra CreamBinti Jambo CreamMalaika Medicated Beauty CreamDera Heart With Hydroquinone CreamNish Medicated CreamIsland Beauty Skin Fade CreamMalibu Medicated CreamCare Plus Fairness CreamTopiclear CreamCarekako Medicated CreamBody Clear CreamA3 Skin Lightening CreamAmbi American FormulaDream SuccessfulSymba Crème Skin Lite ‘N’ SmoothCleartone Skin Toning CreamAmbi Extra Complexion Cream For MenCleartone Extra Skin Toning CreamO’nyi Skin CrèmeA3 Triple Action Cream PearlightElegance Skin LighteningClere CreamClear Touch CreamCrusader Ultra Brand CreamUltime Skin Lightening CreamRico Skin Tone CreamBaraka Skin Lightening CreamFairlady Skin Lightening CreamImmediate Claire Lightening Body CreamJaribu Skin Lightening LotionAmira Skin Lightening LotionA3 Clear Touch Complexion LotionA3 Lemon Skin Lightening LotionKiss LotionPrincess LotionClear Touch LotionSuper Max-Tone LotionNo Mark CreamBody ClearTop ClearUltra ClearPeau Claire Lightening Body OilG &G Dynamiclair LotionG & G Teint UniformeG & G Cream Lightening Beauty CreamDawmy – Lightening Body LotionMaxi White CreamBioclare Lightening Body Lotion
3.2 Vipodozi vingine vyenye Hydroquinone
Fair & White Powder (Exclusive Whitenizer & Serum)New Youth Tinted Vanishing CreamSkin Success Fade Cream RegularTeint Clair Clear Cpmplexion Body LotionMareme CreamSi Clair Plus CreamClair & White Body CreamBody White LotionBio Claire CreamForever Aloe MSM GelKroyons Baby Oil
3.3 Sabuni zenye kiambato cha Hydroquinone
Body Clear Medicated Antiseptic SoapBlackstarCherie Claire Body Beauty Lightening & Treating SoapImmediate Claire Body Beauty SoapLady ClaireG.C Extra ClearTop Clear Beauty Complexion SoapUltra Clear
3.4 Vipodozi vyenye Hydroquinone pamoja na Steroid
Clear Essence Skin Beautifying Milk For Sensitive SkinFair & White Clarifiance Fade CreamFair & White Exclusive Whitenizer Body LotionFair & White Exclusive Whitenizer CreamFair & White Exclusive Whitenizer GelFair & White Maxitone Lightening Lotion Sun BlockFair & White So White Skin Perfect Gel
3.5 Sabuni zenye kiambato cha Mercury (Zebaki) na michanganyo yake
Movate SoapMiki SoapJaribu SoapBinti Jambo SoapAmira SoapMekako SoapRico SoapTura SoapAcura SoapFair LadyEleganceBlock & White Skin Whitener Germicidal Bath SoapRose Beauty SoapMaxi-Tone Soap (Skin Lightening Soap)Margostara Soap (New Tannin)Rusty – Whitening Soap (New Formula)Emani Natural Fair Pearls Soap
3.6 Krimu zenye kiambato cha Mercury na michanganyiko yake
Pimplex Medicated CreamNew Shirley Medicated Cream3.7 Krimu zenye Steroids (Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol,
Dexamethasone nk)
Amira CreamJaribu CreamFair & Lovely Super CreamNeu Clear Cream Plus (Spots Remover)Age Renewal CreamVisible Difference Cream (Neu Clear Spots Remover)Body Clear CreamSivo Clair Fade CreamSkin Balance Lemon CreamPeau Claire CreamSkin Success CreamM & C Dynamic Clair CreamSkin Success Fade CreamFairly White CreamClear Essence CreamMiss Caroline CreamLemonvate CreamMovate CreamSoft & Lovely CreamMediven CreamBody Treatment Cream (Spots Remover)Dark & Lovely CreamSivo Clair CreamMusk – Clear CreamFair & Beautiful CreamBeautiful Beginning CreamDiproson CreamDemovate CreamTop Lemon PlusLemon CreamBeta Lemon CreamTenovate CreamUnic Clear Super CreamTopifram CreamFirst Class Lady Cream
3.8 Vipodozi vingine vyenye kiambato cha Steroid
Fashion Fair Gel PlusHot Movate GelHyprogelMova Gel PlusSecret GelSecret CreamPeau Claire Gel PlusHot Proson GelSkin Success Gel PlusSkin Clear Gel PlusSoft & Beautiful GelSkin Fade Gel PlusUltra – Gel PlusZarina Plus Top GelAction Demovate Gel PlusProsone GelSkin Balance Gel Wrinkle RemoverTCB Gel PlusDemo – Gel PlusRegge Lemon GelUltimate Lady GelTopifram Gel PlusClai & Lovely GelFair & White Serum Exclusive WhitenizerMaxi White Lightening Body MilkMaxitone Cleansing MilkAvoderm CreamNiomre CreamNiomre LotionNyala Lightening Body CreamSi Clair CreamCute Press White Beauty LotionWhite SPA Rose LotionWhite SPA UV Lightening Cream
3.9 Vipodozi vya kupunguza unene vilivyopigwa marufuku
Bio Valley Sliming Gel
3.10 Vipodozi vya nywele vilivyopigwa marufuku
African Gold Super GloSofn Free Hair Foodblue Cap ShampooMarhaba Anti-Dandruff Hair CreamBlue Cap SprayBlue Cap Cream
3.11 Vipodozi vinginevyo vilivyopigwa marufuku
Bio Light CreamSalon Dermaplex Amazon Clay 9Normal To Dry Skin)Beauty Secrets Body CreamSwiss Soft N White Lightening GelWhitening Complex Mask
3.12 Vipodozi Vinavyosababisha muwasho vikitumika karibu na macho
Eye Shadow GelEye Shadow Gel 02Eye Shadow Gel 07Eye Shadow Gel 08Eye Shadow Gel 09Eye Shadow Gel 10
TAHADHARI : VIPODOZI VISIVYO SALAMA VIPO VINGI ZAIDI YA HIVYO AMBAVYO VIMEORODHESHWA HAPO JUU NA VINGINE VINGI ZAIDI VINAWEZA VIKAFIKA SOKONI.
Mara zote kuwa makini na vipodozi na pata taarifa, elimu na ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wataalam wa afya, urembo na vipodozi.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteShukrani za dhati kwa AFYA ZAIDI CONSULTANTS - www.afyazaidi.org
ReplyDeletehttps://afyazaidi.org/2016/09/23/vipodozi-visivyo-salamavilivyopigwa-marufuku-na-madhara-yake/