DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: Wanafunzi wakiri kurubuniwa na madereva wa bodaboda
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
 Wanafunzi wa Sekondari ya Jitegemee wamekiri kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa baadhi yao hurubuniwa na madereva wa boda...

 Wanafunzi wa Sekondari ya Jitegemee wamekiri kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa baadhi yao hurubuniwa na madereva wa bodaboda na bajaji kutokana na shida ya usafiri.

Wanafunzi hao walisema hayo jana kwenye risala ya mahafali ya 32 ya kidato cha nne shuleni hapo  iliyosomwa na mwenzao, Notlice Mahuni.

Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wenzake 322 wanaohitimu kidato hicho mwaka huu, Mahuni alimuomba Makonda kuwasaidia wanafunzi jijini hapa kutatua changamoto ya usafiri kwa sababu wengi huishia kudanganywa na watu hao wakiwamo madereva wa daladala.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top