Shirika la Nyumba la Taifa – NHC limezindua sera mpya ya Mnunuzi Mpangaji, ambapo inamwezesha mnunuzi wa nyumba za bei nafuu kulipa kidogo kidogo kila mwezi ndani ya miaka kumi kabla ya kukabidhiwa umiliki rasmi wa nyumba husika.
Kupitia Sera hiyo ambayo itatekelezwa kwenye mikoa 17 yenye miradi ya nyumba za gharama nafuu, mnunuzi mpangaji atahitajika kulipa malipo ya awali ya asilimia 25 ya thamani ya nyumba anayotarajia kununua na kisha kuendelea na malipo ya kila mwezi kwa miaka kumi ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa sera hiyo jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw NEHEMIA MCHECHU amesema nyumba hizo zenye vyumba viwili zinauzwa thamani ya kati ya milion 29-38 huku nyumba ya vyumba vitatu zikiuzwa kati ya shilingi milion 39-49.
Post a Comment