Unahitaji kujua umebakiwa na siku ngapi za kuishi duniani? Ipo app ya simu itakayokupa jibu hilo Maajabu ya ukuaji wa teknolojia unazalisha stori mpya kila siku ila leo huenda ukashtuka; unajua simu yako inaweza kukwambia siku yako ya kufa?
‘Macabre iPhone App’ ni application ambayo unaweza kuiweka kwenye simu yako na jukumu ambalo utakuwa nalo ni kuweka ratiba zako zote za siku nzima, application hiyo inapiga hesabu halafu inakupa majibu siku zako ngapi zimesalia kuishi duniani.
Kali zaidi ni kwamba majibu utakayopewa ya idadi ya miaka, miezi, wiki, siku na saa itakuwa inaonekana kwenye screen lock, kwa hiyo kila unapotoa lock ya kwenye screen itakuwa inaonekana hapo juu.
Majukumu yako ya siku ndiyo yataakayoamua siku ngapi utaishi.
Application hiyo inapatikana kwa simu za Apple zinazotumia iOS na Windows 8.
Unadhani uko tayari kuitumia application hii?
Home
»
HABARI MCHANGANYIKO
» Unahitaji kujua umebakiwa na siku ngapi za kuishi duniani? Ipo app ya simu itakayokupa jibu hilo…
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment