DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: Watumishi wavuliwa madaraka kwa ubadhirifu wa Mil 180 huko Kondoa
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kondoa limewavua madaraka Afisa Utumishi na Muhasibu mkuu wa wilaya hiyo baada ya kubainika k...

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kondoa limewavua madaraka Afisa Utumishi na Muhasibu mkuu wa wilaya hiyo baada ya kubainika kuhusika na ubadhilifu wa shilingi milioni 180 za miradi ya maendeleo huku likimuagiza Mkurugenzi kumuandikia barua katibu mkuu TAMISEMI kuwahamisha vituo vya kazi maofisa wengine watatu waliotuhumiwa kwenye sakata hilo.

Baraza hilo limefikia maamuzi hayo baada ya kupokea ripoti ya Tume ya uchunguzi iliyoundwa na katibu tawala wa mkoa wa Dodoma kwa maofisa saba wa Halmashauri hiyo waliotuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha hizo na kubaini Muhasibu mkuu Juliana Kirengi na Afisa Utumishi Emmanuel Chinduhuli wakihusika moja kwa moja na ubadhilifu huo hivyo wamekosa sifa za kuendelea kuwa watumishi wa umma.

Wakizungumzia maamuzi hayo baadhi ya madiwani wanasema yatakuwa fundisho kwa watumishi wengine ambao wamekuwa na tabia ya kufuja fedha za umma huku pia wakiomba aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo bwana isdory mwalongo ambaye anatuhumiwa kuhusika lakini mamlaka yake ya uwajibishwaji yako ofisi ya rais TAMISEMI.

Awali katika baraza hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Fales Kibasa amewataka madiwani kuhimiza wananchi kuchangamkia fursa ya serikali kuhamia mkoani Dodoma kwa kujiendeleza kielimu kwani kutakuwepo na ongezeko kubwa la ajira ambazo zinaweza kutwaliwa na watu kutoka nje ya mkoa na kuwaacha wazawa wakiendelea kulalamika.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top