LEO KTK TIBA LISHE :
(TUNDA LA TENDE)
Pamoja na kuwa ni tunda
lenye ladha tamu na nzuri
mdomoni ,
lakini kisayansi pia
limethibitika kusheheni
madini na vitamini lukuki,
hivyo kuwa na faida nyingi
kiafya.
1 . Ukila tende mara kwa
mara , mwili wako utapata
aina mbalimbali za madini na
vitamin za kutosha , ambazo
zinapatikana kwenye tunda hili
maarufu duniani . Katika tende
kuna kiasi kidogo tu cha
mafuta ( fat ) na haina lehemu
( kolestrol) .
2 . Ukila tende, utajipatia kiasi
cha kutosha cha protini na
vitamin B1 , B2 , B3 , B5 , A1 , na
C, virutubisho ambavyo ni
muhimu kwa ustawi wa afya
ya mwili wako kwa ujumla .
3 . Ulaji wa tende huimarisha
na kuboresha mfumo wa
usagaji chakula tumboni ,
hivyo utaondokana na
matatizo ya ukosefu wa choo,
au matatizo ya kupata choo
kigumu kinachosababisha
maumivu wakati wa
kujisaidia . Pia ndani ya tende
kuna virutubisho vya ‘ amino
acids’ ambavyo ni muhimu
mwilini .
4 . Ukila tende, mwili utapata
nguvu na kukuondolea uchovu
ndani ya nusu saa tu, kwa
sababu tende ina virutubisho
vya sukari asilia kama vile
‘glucose ’, ‘sucrose’ na
‘fructose’. Ili kupata faida
zaidi za tende,
changanya na maziwa fresh
kisha kula. Unapojisikia
mchovu, badala ya kunywa
vinywaji baridi vinavyodai
kuongeza nguvu , kula tende,
hata kiasi cha punje tatu
kinatosha . Kwa wafunga
saumu, ndiyo maana
inashauriwa kuanza kufungua
kwa kula tende ili kuurejeshea
mwili wako nguvu iliyopotea
siku nzima .
5 . Tende ina madini pia aina
ya ‘potassium ’ na kiasi kidogo
cha chumvi ( sodium) . Madini
haya husaidia uimarishaji wa
mishipa ya fahamu . Watafiti
wamegundua kwamba ulaji
kiasi wa ‘potassium ’ huweza
kumuepusha mtu na kupatwa
na kiharusi ( stroke ) . Pia tende
husaidia kupunguza lehemu
( cholesterol) mwilini ( LDL
Cholesterol) .
6 . Kwa wale wenye matatizo
ya ugonjwa wa kukauka damu
mwilini ( anemia) , wanaweza
kupata ahueni kwa kula tende
kwa wingi ambayo ina
kiwango cha kutosha cha
madini ya chuma ambayo
huhitajika katika utengenezaji
wa damu mwilini . Wakati vitu
vitamu vingine huozesha
meno, utamu wa tende huzuia
uozaji wa meno.
7 . Kwa tatizo sugu na la muda
mrefu la ukosefu wa choo,
loweka tende za kutosha
kwenye maji kiasi cha lita
moja usiku kucha , kisha
asubuhi changanya maji hayo
pamoja na hizo tende ili upate
juisi nzito, kunywa na choo
kitafunguka na kuwa laini.
8 . Kwa matatizo ya ukosefu
wa nguvu za kiume ,
mchanganyiko maalum wa
tende, maziwa, asali na unga
wa hiriki vinaweza kuondoa
tatizo lako. Chukua kiasi cha
kiganja kimoja cha tende,
loweka kwenye maziwa ya
mbuzi kiasi cha lita moja na
yakae usiku kucha.
Asubuhi , zisage tende hizo
kwenye maziwa hayo hadi
zichangayike, kisha weka asali
kiasi cha vijiko vitatu au vinne
vikubwa pamoja na unga wa
hiriki, kiasi cha nusu kijiko
kidogo. Kisha kunywa
mchangayiko huo kila siku
hadi utakapoona mabadiliko
ya kuridhisha .
9 . Tende ni dawa ya unene,
kwa wale wenye matatizo ya
wembamba wa kupindukia na
wanataka kuongeza uzito, ulaji
wa tende kila siku unaweza
kuwasaidia . Lakini hii ina
maana kwamba, wale
wanaohitaji kupunguza uzito,
ulaji wa tende kwa wingi
hauwezi kuwafaa. Pia tende
husaidia uondoaji wa kilevi
mwilini .
10 . Tende inatibu saratani ya
tumbo. Habari njema kuhusu
tende kama tiba ni kwamba,
haina madhara yoyote kwa
sababu ni dawa asilia na
inafanyakazi vizuri kuliko dawa
za ‘ kizungu’ . Tende vile vile ina
imarisha nuru ya macho na
tatizo la kutokuona usiku
( night blindness ) .
Kwa ujumla faida za tende ni
nyingi na unaweza kuila tende
kwa namna mbalimbali, kama
vile kuchanganya na maziwa,
kuchanganya na mkate au
vitafunwa vingine . Ifanye
tende kuwa sehemu ya mlo
wako wa kila siku ili ujipatie
faida hizi 10 na nyingine zaidi.
Post a Comment