DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: SIMANZI: Mbao FC yampoteza mchezaji, Afia uwanjani.
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC, Khalfan Ismail amefariki baada ya kugongana na kuanguka uwanjani. Mechi hiyo ilikuwa inachezwa k...

Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC, Khalfan Ismail amefariki baada ya kugongana na kuanguka uwanjani.

Mechi hiyo ilikuwa inachezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambako michuano ya vijana chini ya miaka 20 inaendelea.

Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC wakati wakiwania mpira na kuanguka na juhudi za kuokoa maisha yake zilionekana kukakwama.

Wakati mauti yanamkuta Ismail, dakika chache kabla alikuwa amefunga bao dhidi ya Mwadui.

Pamoja na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kagera, taarifa baadaye zilizopatikana zilieleza, Ismail alifariki palepale uwanjani.

UONGOZI WA MALINGUMU BLOG NA DOBS FAMILY TUNATOA POLE KWA WANAMBAO WOTE, WANAMWANZA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top