DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: ​Simu za Android zashambuliwa na Gooligan; 
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Imethibitika kwamba wadukuzi wamefanikiwa kuzishambulia simu karibu milioni moja za Android kwa kutumia kirusi cha Gooligan, kirusi hiki in...


Imethibitika kwamba wadukuzi wamefanikiwa kuzishambulia simu karibu milioni moja za Android kwa kutumia kirusi cha Gooligan, kirusi hiki inasemekana huingia katika simu kupitia App zinazopatikana katika masoko yasiyo rasmi ya Apps.

               Tayari simu milioni moja duniani kote zimethibitika kuathiriwa na Gooligan, katika hizo asilimia 57 zinapatikana katika bara la Asia 19% bara la Amerika na katika bara la Ulaya ni 9% Afrika nzima ni asilimia 19 ya simu zote za android ndio zimeathirika.

              Kirusi hiki kinaingia katika simu baada ya mtumiaji kupakua na ku-install app kutoka katika soko lisilo rasmi( 3rd  party market) na baada ya kuingia katika simu ya mtumiaji app hizi huanza kuiba nywila ambazo unatumia katika kuingia katika mitandao mbalimbali hasa ya Google.

Muonekano wa jinsi gani wadukuzi wanafanikisha shambulizi; hichi ndicho tulichoelezea
Tayari uchunguzi unaonesha kwamba kirusi hiki cha Gooligan kinapatikana katika app zaidi ya 80 ambazo zinapatikana katika masoko yasiyo rasmi, hii ni tishio hasa kwa sisi ambao tunatumia app hizi katika simu zetu.
EPUKA KUPAKUA APPS HIZI KUTOKA MASOKO YASIYO RASMI!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top