WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwa na tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao shuleni na kushirikiana na walimu ili waweze kujua maendeleo ya watoto wao.
Aidha, amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi ya walimu sambamba na kujenga nyumba bora ili kutoa elimu mzuri kwa watoto wao pamoja na kuinua kiwango cha ufaulu.
Majaliwa aliyasema hayo jana wakati akizindua nyumba ya walimu Shule ya Sekondari Oljoro Kata ya Laroi wilayani Arusha.
Alisema baadhi ya wazazi na walezi, hawana tabia ya kukagua madaftari ya watoto wao, wala hawana mawasiliano na walimu ili wajue mienendo ya watoto wao, hali itakayowezesha kujua kama mtoto anaelewa au la Alitoa rai kwa wazazi hao kuchangia baadhi ya michango mengine katika elimu.
Alisema ingawa serikali imefuta baadhi ya michango, mengine inapaswa kuchangiwa ili kuwezesha maendeleo ya shule na elimu.
Awali, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Majaliwa alisisitiza nidhamu ya kazi, ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi inayomkabili wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Alexander Mnyeti alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi. Kwamba baadhi ya mashamba yameorodheshwa ili yaweze kufutiwa hati na kurudishwa kwenye halmashauri hiyo ili wanachi waweze kugawiwa maeneo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema anaandaa semina ya viongozi ili kufundishwa majukumu yao ili kila mtu aheshimu kazi yake Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk, Wilson Mahera alisema Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari ya awamu ya pili (SARPCCO II), umewezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 4, vyoo 20 na vyumba vya madarasa 6.
Post a Comment