DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: Madaktari Kenya wakataa nyongeza ya mishahara ya serikali
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Madaktari Kenya wamegoma tangu mwanzo wa Desemba Madaktari nchini Kenya wamekataa nyongeza ya karibuni zaidi iliyopendekezwa na serikali k...


Madaktari Kenya wamegoma tangu mwanzo wa Desemba

Madaktari nchini Kenya wamekataa nyongeza ya karibuni zaidi iliyopendekezwa na serikali katika juhudi za kujaribu kumaliza mgomo wa madaktari na wahudumu wa afya ambao umedumu kwa mwezi mmoja sasa.

Mgomo huo umelemaza huduma katika hospitali na zahanati za umma.

Rais Uhuru Kenyatta alikutana na wawakilishi wa chama cha taifa cha madaktari hao Jumanne na kupendekeza nyongeza ya mshahara na marupurupu ya madaktarii kwa angalau $560 (£450).

Kenya yapeleka madaktari wa jeshi kuhudumu hospitali za umma

Hilo lingesababisha madaktari wanaoanza kazi kulipwa takriban $2,000 kila mwezi.

Viongozi wa chama hicho, ambao walikuwa wameahidi kutangaza msimamo leo, walisema pendekezo la serikali linawafaa madaktari lakini kuna baadhi ya mambo ya kuwafaa wananchi ambayo yameachwa nje.

Madaktari wanaitaka serikali kutekeleza makubaliano ya mishahara na marupurupu yaliyotiwa saini mwaka 2013.

Kwenye makubaliano hayo, serikali iliahidi kuongeza idadi ya madaktari, kuongeza pesa za utafiti wa kimatibabu, dawa na vifaa na mitambo katika hospitali za umma.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top