DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: Ngoma za usiku ”ngoma za majini” zachangia Mtwara kufanya vibaya kielimu.
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Wadau wa elimu katika mkoa wa Mtwara wamesema upo umuhimu kwa serikali ya mkoa kupiga marufuku ngoma za usiku- maarufu ngoma za majini amb...


Wadau wa elimu katika mkoa wa Mtwara wamesema upo umuhimu kwa serikali ya mkoa kupiga marufuku ngoma za usiku- maarufu ngoma za majini ambazo zimeshamiri katika maeneo ya vijijini sambamba na kuwafuatilia baadhi ya walimu ambao wanatumia muda mwingi kufanya biashara za bodaboda badala ya kufundisha na hivyo kuchangia mkoa kufanya vibaya kielimu.

Wakizungumza na ITV baadhi ya wadau wa elimu katika mkoa wa Mtwara wamesema utafiti uliyofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya mkoani Mtwara kwa kushirikiana na TWAWEZA mwaka 2014-2015 ulibaini kuwa  hali ya elimu katika  baadhi za shule za msingi na sekondari si ya kuridhisha,ikiwemo mazingira ya kufundishia.

Hata hivyo kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Mtwara wamesema ni jambo lisilopendeza kwa mkoa kushika nafasi ya mwisho hivyo kuomba wazazi kufuatilia elimu ya watoto wao.

Mbali na hilo wadau wa elimu katika mkoa wa Mtwara wameiomba serikali ya mkoa kuitisha kongamano litakalokuwa na mjadala mpana kuhusu elimu lengo likiwa kuondoa changamoto zinazochangi kushuka kwa elimu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top