Momba. Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando amewataka waathirika wa mvua iliyoambatana na upepo mkali katika kata za Ivuna na Mkomba Wilayani Momba kukarabati nyumba zao haraka ili kuendelea na kazi za Kilimo kwani mvua za mwaka huu zinazonyesha ni za kusuasua badala ya kusubiri msaada wa kujengewa nyumba zao na Serikali.
Dc Irando aliyasema hayo leo wakati alipowatembelea waathirika hao na kutoa salamu za pole za Serikali kutokana na maafa hayo yaliyowakuta wananchi wa kata hizo.
Akizingumza na waathirika hao kwa nyakati tofauti katika kata hizo, Irando aliwapa pole kwa janga hilo lililowakuta na kuwambia kuwa ndio mipango ya Mungu na wasione kuwa ni mkosi kwao bali waone kuwa ni heri na baraka kwani kazi ya Mungu haina makosa na yeye ndio mpangaji mkuu.
Irando aliwataka waathirika hao kuanza kukarabati nyumba zao na kutokuisubiri Serikali kuja kuwajengea kwani msimamo wa Serikali ni kukarabati na kujenga miundombinu na taasisi zake zilizoharibiwa na mvua hizo.
Post a Comment