DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: UFUGAJI BORA WA  NGURUWE
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
UFUGAJI BORA WA  NGURUWE Mwongozo wa ufugaji bora wa nguruwe kwa mfugaji mdogo, kuzingatia tija, afya na thamani ya mnyama Umetolewa na Mr...

UFUGAJI BORA WA  NGURUWE

Mwongozo wa ufugaji bora wa nguruwe kwa mfugaji mdogo, kuzingatia tija, afya na thamani ya mnyama
Umetolewa na Mradi wa SLIPP wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro, Tanzania kupitia Ufadhili wa DANIDA

Watayarishaji:
Profesa Faustine P. Lekule Profesa Amandus Muhairwa Dr. Helena Ngowi
Dr. Daniel Mushi
Dr. Eliakunda Casmir Kimbi

Mchoraji
Simon John Rwegayura

1. Utangulizi
Ufugaji wa Nguruwe ni kati ya shughuli zinazokuwa haraka katika Afrika Mashariki na ya Kusini. Ukuaji wa miji na ongezeko la watu kumeendana na ongezeko kubwa la mahitaji ya protini ya wanyama. Uwezo wa kukua haraka, ubora wa nyama kiafya na ladha nzuri inatoa nafasi kubwa ya maendeleo ya ufugaji wa nguruwe kama chanzo cha kipato kwa mfugaji. Kijarida hiki kinatoa mwongozo kuhusu mahitaji muhimu ya ufugaji nguruwe, mbinu za kuboresha uzalishaji, kudhibiti magonjwa na pia mwongozo wa kujali haki za nguruwe kama kiumbe hai kinachoweza kusikia maumivu kisipotendewa kinavyostahili. Nguruwe ana gharama ndogo za matunzo, anatoa mafuta, huleta kipato cha pesa, hutoa mbolea ya mimea. Faida ya ufugaji nguruwe hutegemea zaidi ubora wa matunzo. Vile vile kumbuka kutumia vyanzo nafuu vya chakula na kujengea miudombinu. Msomaji anashauriwa kuwaona wataalamu kwa ushauri zaidi na pia kusoma vitabu vya rejea kuhusu ufugaji nguruwe.
2. Ukweli kuhusu Nguruwe
Nguruwe ni rnnyama msafi sana na mwenye akili. Akipewa banda lenye nafasi ya kutosha huweza kuchagua sehemu ya kulala, kujisaidia na akauweka mwili wake katika hali ya usafi sana. Usafi wa banda na mazingira utakuhakikishia nguruwe wasafi bila uchafuzi wa mazingira kama tunavyoona kwa wafugaji wengi mijini na vijijini. Tenga mavazi na viatu maalumu kwa ajili ya kazi za nguruwe na oga vizuri baada ya kufanya kazi kwenye mabanda ya nguruwe kwa muda mrefu.
3. Nyumba ya nguruwe
Kwa ujumla nyumba za aina mbili huhitajika katika ufugaji wa nguruwe
o Nyumba za kukuzia na kunenepesha nguruwe wa kuchinja
o Nyumba za nguruwe wazazi

Sifa za msingi za nyumba bora ya nguruwe
• yumba ijengwe eneo lenye kivuli cha kutosha
• yumba iwe na nafasi ya kutosha
• Ijengwe sehemu yenye mwinuko kiasi iii kuwezesha maji kuondoka kwa urahisi
• Iwe na chombo/kihori cha kuweka chakula na kingine chakuweka maji
• Iwe na sakafu imara iliyotengenezwa kwa saruji, mabanzi, miti na isiwe na unyevu
• Sakafu ya saruji iwe na mteremko (slope) inayoweza kuondoa uchafu kwa urahisi ndani ya banda.
• Sakafu ya mabanzi, mbao au miti iwe inatoa nafasi ya kuondoa uchafu kama kinyesi ndani ya banda.
• Iwe na mtaro wa kuondolea maji, mkojo na kinyesi hadi shimo la kutunzia
• Kuta za mabanda ya nguruwe zinatakiwa kuwa imara, ziwe na uwezo wa kuwasitiri nguruwe wasitoke nje.
• Iweze kuingiza hewa ya kutosha ndani ya banda hasa kama ukuta umezibwa (solid walls)

2

• Paa linaweza kupauliwa vizuri kwa nyasi, makuti, bati n.k kama inavyoonekana hapa chini

Picha namba 1 Picha namba 2
Mabanda kwa ajili ya nguruwe wanne wenye umri wa miezi minne hadi mitano. Vipimo rya banda: 2 x 2.5 m.  Zingata vipimo viliryoonyeshwa iii k:uruhusu hewa k:upita na k:uwapa nguruwe nafasi ya k:utosha

Banda hili hapa chini limejengwa kwa ajili ya mama nguruwe na watoto. Vipimo: ukubwa wa banda
= 2 x 2 m, ukubwa wa sehemu ya mama nguruwe = 0.6 x 0.6, sehemu ya watoto = 0.6 x 0.6 m

4. Upate wapi Nguruwe wa Kufuga
Nunua nguruwe wa kufuga kutoka kwenye mashamba au wafu,,,craji wanaoaminika ukizingatia yafuatayo.
• Usizalishe nguruwe wanaotokana na ukoo mmoja yaani ndll::,oU kama kaka ria dada. Nunua dume najike toka mahali   tofauti.
• Tumia ushauri wa wataalamu kuchagua 11c,auruwe bora

Sifa za kuangalia kwa nguruwe bora wa mbegu:
• Nguruwe wa mbegu awe na sifa ya kukua hara.ka na asiwe na ulemavu wa aina yeyote, na hasa wa miguu kwa dume.
• Mama mzazi wa nguruwe awe na historia ya k..u.aa watoto 10 hadi 12 kwa mzao mmoja
• Jike awe na chuchu zaidi ya 12.
• Dume awe na sehemu za kiume yaani korodani na uume unaoonekana sawa sawa. Pia awe na hamu ya kupanda majike.

5. Mbinu za uzalishaji
Matunzo ya dome la uzalishaji
• Chagua dume la mbegu bora, lisilokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Tenganisha dume na majike iii kuepusha kupandwa kusiko na kumbukumbu. Dume la nguruwe halipaswi kunenepa, kwa hiyo usimlishe chakula kingi na mpatie mazoezi ya kutosha asije akawa mvivu
• Nguruwe dume anaanza kupanda majike akiwa na umri wa miezi 4 hadi miezi 9. Dume liruhusiwe kupanda mara moja tu kwa kila juma. Anapofika miezi 10 anaweza kupanda mara mbili hadi mara tatu kwa wiki. Akiwa na mwaka mmoja na zaidi anaweza kupanda kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa majuma mawili. Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande majike 15 hadi 20 kwa mwaka.
• Madume madogo yapande majike madogo, dume kubwa likimpanda jike <logo anaweza akamletea maradhi ya mgongo. Ni muhimu kupandisha dume kabla hajala chakula, na asitumiwe mara tu baada ya chakula iii asiwe mvivu.

Utunzaji nguruwe mwenye mimba
• Mimba ya nguruwe huchukuwa rniezi mitatu (3) wiki tatu(3) na siku tatu(3) yaani siku 114
• Nguruwe mwenye mimba apewe chakula cha kutosha kiongezwe polepole tokea posho ya kawaida hadi kilo 3 - 3.5 kwa siku.

Matayarisho ya nyumba kabla ya  kuzaa
• Osha banda la kuzalia kwa maji na kuliacha likauke
• Tandika nyasi kavu mara baada ya nyumba kukauka
• Ongeza taa ya chemli au umeme kama uko mikoa yenye baridi kwenye sehemu ya vitoto.
• Tengeneza sehemu ya kuzalia kwa mbao au mabomba (Tazama picha namba 3)

Kumuandaa nguruwe mama kabla ya  kuzaa
• Mpe  dawa ya minyoo siku 10 kabla ya kuzaa
• Mogeshe mama nguruwe kwa sabuni ya mkono na brashi
• Muhamishie katika churnba cha kuzalia siku 7 kabla hajazaa
• Mpunguzie lishe siku 2 kabla  ya kuzaa
• Siku ya kuzaa mpe nguruwe maji ya kunywa tu
Matunzo ya vitoto vya nguruwe
Vitoto vya nguruwe vinyonye maziwa ya mama siku zote hadi wakifikisha siku 56. Mambo muhimu ya kufanya kwa vitoto vya nguruwe yameainishwa kwenye jedwali namba 1 hapa chini:

Jedwali namba 1: Mambo muhimu ya kufanya kwa vitoto l:)}Q nl(uruwe
   

Upandishaji jike
• Kati ya siku nne hadi saba baada ya kuachishwa watoto, nguruwe mama hupata joto. Nguruwe jike alie kwenye joto apelekwe kwenye banda la dume na sio kinyume chake. Rudia kumpandishajike alie kwenye joto masaa 12 baada ya mpando wa kwanza; rudia kumpandisha mara 2 hadi 4. Kamajike hatarudia kwenye joto baada ya wiki 3 atakuwa ameshika mimba.

Dalili za joto
• Sehemu ya uzazi kubadilika na kuwa nyekundu
• Nguruwe hatulii na hukojoa mara kwa mara
• Ute kama makamasi hutoka sehemu za siri
• Nguruwe mwenye joto hujaribu kuwapanda wenzake na yeye akipandwa hutulia

6. UTUNZAJI WA VITOTO VYA NGURUWE.

Ulishaji wa maziwa ya kwanza
Baada ya kuzaliwa na kusafishwa, hakikisha vitoto vinanyonyeshwa. \ 1t0Y,u •iwekewedawa (Iodine 5%) iii kuzuia magonjwa. Kama mama amefariki mara tu baada ya kuzaa na hakuna nguruwe mwingine anayeweza kunyonyesha; tumia maziwa ya ng'ombe. ongeza sukari na yai bichi koroga na uwanyonyeshe kwa kutumia chupa ya maziwa ya mtoto.

Joto
Vitoto vya nguruwe havizaliwi na manyoya na hawana mafuta mengi ya kutosha kuwaletea joto mwilini; hivyo ni rahisi kufa kwa baridi. Tumia taa ya stimu au chemli kuongeza joto.

Kuzuia upungufu wa damu
Maziwa ya nguruwe yana upungufu wa madini ya chuma yaongezayo damu. Hivyo baada ya majuma mawili au matatu watoto huanza b..-udhoofu kwa kukosa madini hayo mwilini. Kuondoa tatizo hili inabidi vitoto vidungwe sindano ya madini l,..•wenye misuli siku mbili au tatu tangu kuzaliwa. Kama sindano haipatikani njia nyingine za kuwaparia watoto madini hayo ni kwa kuwapa vidonge vya madini chuma, au kuwapa madini hayo kwen_ e   dimi z.ao au chuchu za mama yao siku mbila hadi tatu baada ya kuzaliwa.

Ukataji meno
Siku chache kabla ya kuzaliwa, meno yaliochongoka • Meno hayo humuumiza mama wakati watoto wanapo n:, mateke. Hii husababisha vifo vya watoto kutokana na k -"= - inabidi meno hayo yakatwe  na chombo kinachofanana kupunguza madhara hayo. Muone bwana mifugo kwa mae

oz.a  tika taya mbili.
e mama hupiga watoto •
•osa mazi\\ ya mwanzo. Hiyo si (Tazarna  picha namba 4), ili

5

Kulisha chakula cha ziada
Chakula kigumu zaidi ya maziwa kianze kulishwa kidogo k:idogo kuanzia siku ya kumi baada ya kuzaliwa, kwani wakati huu maziwa ya mama hayatoshelezi. Endelea kuwapa chakula hiki mpaka watakapo zoea kutokunywa maziwa ya mama yao tena. Chakula hiki kiwe na viini lishe  vya kujenga mwili, kuleta nguvu na kuzui maradhi. Nguruwe wapewe chakula hiki kwa wingi na maji ya kutosha.

Kuhasi
Vitoto ambavyo havihitajiki kwa ajili ya kizazi bora katika mfugo, vihasiwe vikiwa katika juma la tatu hadi la nne. Nguruwe walio hasiwa huwa wapole, wenye nguvu, wazito na nyama yao haina harufu ya dume. Bwana mifugo atakupa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya.

Kuachisha kunyonyesha
• Viachishe vitoto kunyonya wakifikia umri wa miezi miwili wanapokuwa na uzito wa kilo 10.
• Siku ya kuachisha kunyoyesha muondoe mama nguruwe kwa watoto wake na kumuweka chumba kingine
• Mpe mama chakula cha kutosha

7. Vyakula na ulishaji
Chakula bora kwa nguruwe ni moja ya mahitaji muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha nguruwe kinagharimu yapata asilimia hamsini sabini ya gharama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija  na ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe duni. Nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.

B. Baadhi ya faida za lishe bora kwa nguruwe  ni:
1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa nguruwe na hivyo kupata uzito unaohitajika kwa kipindi k:ifupi .
2. Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji kwa sababu nguruwe atahitaji k:iasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito mkubwa
3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivi shwa na mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda

C. Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe
Nguruwe wana uwezo wa kula aina nyingi za vyakula lakini vyenye uwezo wa kumeng'enywa kwa urahisi. Chakula cha nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni
1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (kama pumba za mahindi, ngano, mchele)
2. Vyakula vya kujenga mwili (kama mashudu ya alizeti, pamba, unga wa dagaa)
3. Vyakula vya asili ya madini (kama chumvi, chokaa, mifupa iliosagwa)
4. Vyakula vya asili ya vitamini (kama majani mabichi, mbogamboga na matunda)
5. Maji
6

D. Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe
Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:
• Mchanganyiko wake uwe na viinilishe vinne vilivyotajwa hapo juu
• Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwenye mazingira yako
• Aina ya mchanganyiko wa chakula ni muhimu uzingatie mahitaji ya nguruwe kama umri (mfano: nguruwe wanaonyonya, waliochishwa kunyonya, wanaokua, na  wanaonyonyesha)

Mfano jedwali Na 2 linaonyesha michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.
1. Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa wafugaji walioko kwenye mazingira ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
2. Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga machicha ya pombe na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi.
3. Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao pumba za mpunga na mahindi yanapatikana kwa urahisi.

Jedwali namba 2: Michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe
Na Aina ya viinilishe Michan2anyiko (Asilimia)
Namba 1 Namba2 Namba4
1 Vyakula vya wanga
1. Pumba za mahindi
2. Pumba laini za mpunga
3. Machicha ya pombe yaliyokaushwa
4. Mahindi yaliyobarazwa
70.25 32 30.00
- 25 33.00
- 21 -
- - 10.00
2 Vyakula vya protini
A. Protini ya nafaka
1. Mashudu ya alizeti 2.Mashudu ya michikichi
3. Soya iliyochemswa na kubarazwa
B. Protini ya Wanyama 4.Unga wa dagaa/samaki 5.Damu iliyokaushwa
22.00 14 22.00
-
- -
-
-

4.00
-
2.00
2.25
3.25
-
3 Vyakula vya asili vya madini
1. Chumvi ya mezani
2. Chokaa ya mifugo
3. Unga wa mifupa
4. Madini na vitamini mchanganyiko
0.50 0.50 0.50
2.00 2.00 2.00
1.00 1.00 1.00
0.25 0.25 0.25
Jumla 100. 100 100.

7

E. Kiasi na namna ya kulisha
• Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula mara mbili (asubuhi na mchana) au zaidi kwa siku
• Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na rika tofauti kimeonyeshwa kwenye    jedwali
Namba3
• Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji wanashauriwa kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya kijadi karna vyakula vya ziada mfano, majani mabichi laini, majani ya maboga, mbogamboga, matunda kama maparachichi, majani ya viazi n.k.

Jedwali na 3: Viwango vya kulisha nguruwe wa uzito mbalimbali
Na Wakati Uzito wa nguruwe (kilo) Kiasi cha chakula (kilo kwa siku)
1. Baada ya kuachishwa 10-17 0.75
kunyonya hadi uzito kiasi
2. Uzito uliozidi kiasi kidogo 18 - 29 1.00
3. Uzito wa kawaida 30- 40 1.50
4. Uzito mkubwa kiasi 41 - 60 2.00
5. Uzito mkubwa 61 - 80 2.5
6. Uzito mkubwa sana 81 - 100 3.00
7. Nguruwe anaye nyonyesha 120 - 150 6.00

Jinsi ya kulisha jike la nguruwe  kabla na baada ya  kuzaa
1. Kipindi cha mimba, kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha
1.1 Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa
• Apatiwe chakula kiasi karna kilo mbili kwa siku
• Kiasi hik:i kiendelee hadi wik:i 3 kabla ya kuzaa

1.2 Wiki tatu kabla ya kuzaa
• Ongeza chakula kufikia kilo mbili na nusu.

1.3 Wiki moja kabla ya kuzaa
• Anza kuopunguza chakula taratibu hasa vyakula vya nafaka (Concentrate rations).
• Ongeza vyakula vya   mbogamboga,  majani laini na matunda (laxative  meals).

1.4 Siku ya kuzaa
• Usimpe chakula chochote cha nafaka.
• M pe vyakula vya mbogamboga,na vilaini kwa kiasi kidogo tu
• Mpatie maji ya kutosha.

1.5 Siku ya 1 -  2 baada ya kuzaa
• Mpe nusu kilo ya chakula karnilifu.

1.6 Siku ya 3 na kuendelea
• Ongeza chakula cha nafaka kwa kiasi cha kilo 1 kwa siku.
• Ongeza kufikia kiwango kinachohitajika kulingana na idadi ya watoto alionao mama nguruwe.

Zingatia
• Mama nguruwe anahitaji kilo 3 za chakula kwa matumizi yake ya kawaida.
• Atahitaji kiasi cha ziada cha theluthi moja (1/3) ya kilo ya chakula kwa kila mtoto aliyenae

Mfano: kama mama ana watoto 9 atahitaii kiasi  ani cha chakula?
Mahitaji mama peke yake Mahitaji kutokana na watoto Kiasi cha chakula kwa siku
3kg Theluthi moja x 9: (113    X   9 =
3 Kg) 3 kg + 3 kg = Kilo 6 kwa siku
Endelea kumpa kiwango hicho cha chakula mpaka ifikapo wik:i moja kabla ya kuwaachisha watoto kunyonya.
Wiki moja kabla ya kuwachisha punguza kiwango taratibu mpaka kufik:ia kilo 31•2 J...'Wa siku.

Baada ya kuachisha kunyonya
• Mama nguruwe wapatiwe chakula bora kilicho na kiwango kikubwa cha maclini na vitamini kiwango cha kilo 2 - 3 kwa siku.
• Hii itamsaidia kuivisha mayai, hivyo kumsaidia kupata joto mapema.

8. Magonjwa na Afya
Magonjwa yafuatayo ya nguruwe yameelezwa kifupi:-Ili kumpa mfugaji maarifa ya kutambua na kuzuia /kutibu. Waone wataalamu ukiona dalili hizi
Dalili Ugonjwa Udhibitiffiba
Homa kali, kukosa raha na kuwa mkali kwa watoto Ukosefu wa maziwa Mama nguruwe atibiwe kwa antibiotiki kama na homa. Mtalamu akague chuchu kuona kama zina matatizo ya kuzaliwa. Kagua meno ya vichanga kama hayajakwatwa yakatwe.
Uharo wa njano nguruwe akiwa na umri wa wiki 3 Kuharakwa nguruwe wachanga Tibu kwa antibiotiki.
Safisha Banda, vyombo na mazingira kila mara kuua vimelea kwenye mazingjra
Malengelenge ya mafua puani mdomoni, chuchu na kwato Ugonjwa wa miguuna midomo Ugonjwa hauna tiba maalumu. Osha vidonda kwa dawa ya kuua vimelea vya magonjwa
Vifo vya ghafla damu puani na sehemu ya kutolea kinyesi Kimeta Toa taarifa haraka k\va mtaalamu aliye karibu. k\vani nyama ya nguruwe hawa haifai J...'Uliwa.
Kujikuna katika vizingiti na kuharibika ngozi Ukurutu Sindano ya Ivermectin kwa IIe,oUIUWe wote. Rudia baada ya wiki 2
Joto kali, vifo vingi sana kushindwa kutembea, kutokula. Homa ya nguruwe Hakuna dawa, toa ripoti k\va mtaalamu iii taratibu za udhibiti zifuatwe.

(\

9. Matunzo na udhibiti na haki za msingi
Kushika na kuongoza nguruwe
guruwe anapaswa kuanza kushikwa tokea akiwa mdogo iii azoane vema na binadamu. Mfugaji anapaswa kujifunza jinsi ya kushika, kuongoza na kumuangusha nguruwe bila kusababisha maumivu au msongo kwa mnyama.

1. Kubeba nguruwe mtoto
Mkamate nguruwe mtoto kwa kukamata miguu ya nyuma, mnyanyue na kuweka mkono mwingine chini ya tumbo lake kama ilivyoonyeshwa kwenye picha. Hapo utaweza kumtibu, kumhamisha au hata kumkagua kama ana tatizo.

Picha namba 5

2. Kumuongoza  nguruwe mkubwa
Kumuongoza nguruwe aende unapotaka inawezekana iwapo utatoa ubao wa kuongozea nguruwe. Ubao huo wenye upana sentimeta 80 na urefu wa sentimeta 80 unaweza kutengenezwa kwa kutumia mlango wa zamani au mbao za gharama ndogo. Mkinge nguruwe na ubao mmoja kila upande kulia na kushoto huku ukiacha nafasi ndogo ya kumruhusu kuona upande wa kichwani, fanya hivyo huku ukimuelekeza upande unaotaka aende. Unaweza kumuongoza nguruwe kwa ubao mmoja (picha na 6) iwapo kuna nafasi ya kumkinga kulia na kushoto kama ilivyoonyeshwa.

3. Kudhibiti nguruwe wakubwa

Picha namba 6

Picha namba 7

Tumia kamba ya katani iliyosukwa au waya wa kukamatia nguruwe (pig snare). Nguruwe akifungwa kamba ya kitanzi katika taya la juu la mdoma na kuvutwa kuelekea mbele, yeye atavuta kuelekea nyuma kama ilivyoonyeshwa katika picha namba 7, Mbinu hii huwezesha kumkagua nguruwe, kumchoma sindano, kumuogesha au hata kuruhusu kumfunga kamba miguuni ili kumuangusha.

4. Kumuangusha chini nguruwe
Kuangusha chini nguruwe, mfunge kamba mdomoni kama ilivyoonyeshwa hapo juu (Picha namba 8).
Kisha funga miguu ya mbele pamoja kwa kamba moja, na miguu ya nyuma ifungwe kwa kamba nyingine. Mtu mmoja abakie kudhibiti kamba ya mdomoni ili nguruwe asitembee, mtu wa pili avute kamba za miguu moja moja huku akiwa amesimama (angalia picha) upande wa pili tokea zinapotokea kamba chini ya tumbo la nguruwe, Huyu avute zile kamba kila moja katika mkono tofauti, nguruwe ataanguka chini. Funga miguu vizuri  kudhibiti
nguruwe asiinuke. Picha namba 8

10. Kulinda haki za nguruwe
a. Usimpige nguruwe kwa sababu yeyote ile
         b. Usiwajaze nguruwe kwenye chumba kidogo kisicho na nafasi ya kutosha watapigana, watachafuka, na kuumizana
c. Usimuache nguruwe juani, nguruwe hatoki jasho joto litamtesa na hata kumuua
d. Usiweke madume wawili chumba kimoja hasa kama hawafahamiani, watapigana sana.
e. Usisafirishe nguruwe kwenye gari lisilo na nafasi ya kutosha na wasafirishajijioni na asubuhi wakati hamnajoto
Fanya haya
a. Wape nguruwe nafasi ya kutosha kama ilivyoelekezwa katikajarida hili.
b. Wape chakula na maji ya kunywa ya kutosha
c. Nguruwe akiugua apewe tiba mara moja ili kuepusha maumivu yasiyo ya lazima
d. Chinja nguruwe kwa taratibu zilizoelekezwa ili kumuepusha na kifo cha mateso

11

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top