DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: J.k Nyerere na wanaotesa au kuwanyanyasa wananchi..
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
NUKUU ZA NYERERE Mara nyingi mno viongozi katika serikali na watumishi wa Serikali, na hata viongozi wa chama, wanashindwa kuonyesha kwa vi...

NUKUU ZA NYERERE
Mara nyingi mno viongozi katika serikali na watumishi wa Serikali, na hata viongozi wa chama, wanashindwa kuonyesha kwa vitendo vyao kwamba wanajali watu.
Hawajitahidi kuwasaidia watu binafsi ambao wamo katika matatizo hata kama hili linaeeza kufanyika bila ya kuharibu siasa yetu au usalama wetu.

Kuna mifano ya wananchi wetu kuteswa na viongozi wa serikali na wa chama ambao walitarajiwa kuwahudumia wananchi. Na wakati vitendo hivyo vya ukatili vinapoanza kujulikana ,juhudi kubwa zinafanywa kuwanyamazisha ama wale walioteswa ama wale waliojipiga vifua kutoa habari badala yao.
Haya ni mambo ya aibu . Lazima katika jambo hili Chama chetu kiwe macho sana.

Azimio la Arusha baada ya miaka 10 (uk. 44)
Julius K. Nyerere. 1977

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top