UNAKWEPA KULA BAMIA? HIZI HAPA FAIDA ZAKE….
Bamia ni mboga ambayo inafahamika na watu wengi na imekuwa ikitumiwa na watu wengi hapa nchini Tanzania.
Pamoja na bamia kuwa mboga, lakini pia ina faida nyingi katika miili yetu, licha ya kuwa wengi wetu huwa hatufahamu faida zake zaidi ya kula tu kama mboga.
Miongoni mwa faida za mboga hii ni pamoja na kusaidia kuondosha vimelea vya sumu kwenye ngozi, inasaidia pia kuimarisha afya ya nywele na kuongeza kinga ya mwili.
-Bamia husaidia kuondoa uchovu wa mwili na msongo wa mawazo pamoja na kusaidia kutibu tatizo la kukosa choo.
Aidha, bamia pia inaelezwa kusaidia kusafisha damu, kutibu mafua, vidonda vya tumbo, inaimarisha mifupa pamoja na kuwa kinga ya magonjwa kama utapiamlo na anemia.
Ni msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya mifupa au maumivu ya viungo kwani huongeza uteute kwenye viungo vya mifupa, ili upate faida hii inakupasa ule bamia kama supu/mchemsho
Mbali na hayo bamia pia inasaidia kutibu magonjwa mbalimbali ya zinaa kama vile kaswende na kisonono. Vilevile inaponya tatizo la kwenda hedhi mara kwa mara na chango la kike.
Hizo ni baadhi ya faida za ulaji wa bamia, endapo utaendelea kutembelea tovuti hii mara kwa mara basi utazidi kupata elimu zaidi juu ya namna vyakula mbalimbali na mimea vinavyoweza kuwa tiba nzuri na kinga ya magonjwa.
Post a Comment