UFANYE NINI TAIRI LIKIPASUKA (BASTI)??
Kuna hatua 6 za kufuata ndani ya dakika 2 tangu kupasuka tairi ambazo unapaswa kuzifuata.
1. USIHAMAKI wala *Kukanyaga Breki*, tulia kwanza kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.
2. KAMATA USUKANI Kwa nguvu kwa mikono yote miwili, USIPINDEPINDE KONA huku ukiwa makini na barabara na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako, ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.
3. ONGEZA MWENDO wa wastani ili kudhibiti mwenendo wa gari. Hivyo kama ulikuwa umekanyaga mafuta usiondoe mguu haraka kwenye hiyo pedo.
4.ONDOA mguu wako taratibu kwenye mafuta USIJARIBU KABISA KUKANYAGA BREKI,Ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari.
Ilhali kama usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.
5. ONDOA gia zote na uziweke kwenye neutral(free) huku bado ukiwa umeshikilia vema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.
6. Baada ya muda mfupi, kulingana na mwendo wako, gari ikiwa imefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kandoni mwa barabara ili usimame.
7. Hatimaye, itakuwa salama zaidi kusimamisha gari lako na kuzima injini.
Hapo utakuwa umeokoa maisha yako na ya abiria wako kutoka kifo.
NYONGEZA: Inapotokea tairi imepasuka ni mara 10 salama kuongeza mwendo kuliko kuhamisha mguu na kukanyaga breki.
Source:
(RSA TANZANIA
Post a Comment