DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: Mwamuzi Jonasia Rukyaa azawadiwa gari
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo amemkabidhi Mwamuzi kutoka Tanzania Jonasia Rukyaa funguo ya gari alilozawadiwa ...

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo amemkabidhi Mwamuzi kutoka Tanzania Jonasia Rukyaa funguo ya gari alilozawadiwa kwa kuchezesha vizuri katika fainali za wanawake barani Afrika, zilizofanyika nchini Cameroon hivi karibuni.

Taarifa ya TFF imesema kuwa wadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye alipangwa kuchezesha michuano hiyo iliyomalizika kwa timu ya wanawake ya Nigeria kuibuka na ubingwa.
Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka.
Alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.

Rais wa TFF Jamal Malinzi amekabidhi zawadi hiyo kwa mwamuzi Jonasia Rukyaa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top