DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: THE TWENTY FOUR HOURS OPERATION IN ENTEBE
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
     Pengine umekuwa ukisikia kisa hiki maarufu duniani cha Idi Amin kuiteka ndege ya shirika la usafirishaji la Ufaransa na kisha kuwatwaa...


     Pengine umekuwa ukisikia kisa hiki maarufu duniani cha Idi Amin kuiteka ndege ya shirika la usafirishaji la Ufaransa na kisha kuwatwaa na kuwaweka kizuizini Wayahudi wapatao 37 pale Entebe international airport. Lakini huenda hujui ni nini kilitokea na ilikuwakuwaje.

Tutajaribu kukupa kisa hicho kwa ufupi sana! Nyuma ya utekaji ule inasemekana alikuwepo Carlos, mvenezuela na gaidi la kimataifa la nyakati hizo. Baada ya utekaji ule, Amin alimwambia waziri mkuu wa Israel, haachie huru wafungwa kadhaa wa Kipalesitina, naye atawaachia huru mateka wale wa Kiyahudi.

Kama unavyojua, Wayahudi huwa hawasalimu amri hata siku moja. Waziri mkuu wa Israel alimufuata kamanda mmoja msitaafu wa Kiyahudi aliyeitwa Jonathan Netanyau, alimukuta shambani, "Bw Jonathan kama unavyojua, dada zetu na kaka zetu wametekwa pale Entebe, sasa ninakupa operesheni ya kwenda kuwakomboa, wewe ndiwe utakuwa kamanda mkuu wa operesheni hiyo ya kihistoria," alimaliza waziri mkuu wa Israel.

Ikafika zamu ya Jonathan Netanyau kumujibu waziri, "mzee hiyo operesheni tayari umeifikisha  kwa wanaume, ninakuhakikishia nitafanya operesheni ya kihistoria na kila atakayeisikia basi masikio yatamuwasha!!" alijibu kamanda msitaafu aliyekuwa amevaa jinzi ya blue, t-shirt nzito ya sweta, pistol ikininginia karibu na mshipi, akiwa amefuga nywele aina ya Afro, miwani myeusi machoni, na mda wote alikuwa akivuta kiko!

Walipeana mikono kuashiria muafaka kufikiwa, na akamwambia waziri mkuu, "ninaomba Vijana waliotoka depo wapatao 600, ili niwachuje kupata 400, bora, kisha nitawachuja tena ili kupata 200, nao nitawachuja tena ili kupata 60, na mwisho nitawachuja ili kupata 21 nitakaoenda nao Entebe, kamanda alipewa makomando hao wa Kiyahudi waliokuwa wamefuzu mafunzo ya kijeshi ya jangwani.

Waliingia sehemu moja karibu na mji wa Yeriko, wakajenga majengo ya mda, maarufu kama (temporally buildings) yayaliyokuwa yanafanana kabisa kabisa na gereza la Entebe Uganda, wakaweka na ulinzi kama uleule uliokuwa Entebe, kisha wakawa wanafanya mazoezi ya kupavamia.Mbinu hiyo ya ki jasusi inaitwaga (Original kavu)!!

Ina maana ukifanikisha hapo, hata Entebe utafanikiwa. Yalipigwa mazoezi makali ya kijeshi! Kama kawaida yao, wayahudi huwa hawatumii risasi za bandia ktk mazoezi, hutumia risasi za moto!!! Usipoikwepa unakwenda na maji.

Baada ya wiki moja, kamanda alipeleka ripoti kwa waziri mkuu, kama ifuatavyo, "Mzee tumepiga zoezi na inaonekana askari wapatao Sita wa Kiyahudi watafia pale Entebe. Hapana! hapana!! waziri mkuu alijibu," kupoteza askari Sita wa Kiyahudi ni afadhali mateka wote 37 wapotee, kuliko kupoteza askari Sita wa Kiyahudi, hiyo ni idadi kubwa sana, nenda ujaribu kuipunguza,, "aliongeza waziri mkuu.

Baada ya siku nne kamanda alirudisha taarifa," mzee tumeongeza mazoezi, inaonekana askari wawili wa Kiyahudi watauawa pale Entebe, , "alisema kamanda," bado hiyo ni idadi kubwa, kupoteza askari wawili wa Kiyahudi nafuu tupoteze mateka wote "alisema waziri mkuu,," ngoja ni jaribu kupunguza tena "alijibu kamanda.

Siku tatu baadae akarudisha majibu" mzee inaonekana askari mmoja atakufa, alisema kamanda. Nenda mpige zoezi muone nani atakayekufa, "aliamuru waziri mkuu.

Baada ya siku mbili kamanda alirudisha taarifa tena." Mzee tumepiga zoezi, inaonekana mimi ndiye nitakayekufa "alisema kamanda, Kitu gani kitakuponza?? aliuliza waziri mkuu!! Ni kwasababu kamanda yeyote wa Kiyahudi, huwa wa kwanza kuteremka kwenye ndege na huwa wa mwisho kupanda kwenye ndege!!

Itaendelea.........

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top