DobsFoundation  DobsFoundation Author
Title: THE TWENTY FOUR HOURS OPERATION IN ENTEBE 2.
Author: DobsFoundation
Rating 5 of 5 Des:
ilipoishia, "Kamanda wa Kiyahudi huwa wa kwanza kuteremka kwenye ndege na huwa wa mwisho kupanda kwenye ndege, hivyo basi, mzee nitapin...

ilipoishia, "Kamanda wa Kiyahudi huwa wa kwanza kuteremka kwenye ndege na huwa wa mwisho kupanda kwenye ndege, hivyo basi, mzee nitapingwa risasi wakati ninapanda kuondoka!! Alitoa maelezo kamanda.

Unaonaje, tuiongezee mda wa operesheni?? Aliuliza waziri mkuu! Mzee kufa mimi siogopi!! Kwanza niliapa kulilinda taifa langu la Israel kwa gharama yoyote, pili mwanaume yeyote wa kweli hufa akiipigania familia yake, na mwisho iwapo nikiahirisha, tuna watoto wa kike makomando hapa Jerusalem, wakisikia nimeogopa, haraka sana watachukua jukumu nililolikimbia, wataongoza operesheni vizuri sana pale Entebe na watawakomboa mateka, mimi nitadharilika, lazima niende Entebe mzee "alimaliza kamanda, huku macho yake madogo yakizidi kuzama ndani ya nyusi na kuonekana madogo zaidi!

Siku ya siku ilifika, makomando wote wa Kiyahudi 21 ambao wangeshiriki operesheni hiyo walikaguliwa barabara! Ikiwemo record zao, ni wepesi kiasi gani na hali ya afya yao. Ktk kikosi hicho cha special force inasemekana walikuwemo askari wanne wa kike, na sababu kubwa ya kuwemo askari hao wane wa kike, inasemekana mapigo ya moyo ya mwanamke hudunda taratibu. Hivyo ni vigumu askari wa kike kupoteza shabaha,.

Na asubuhi ya siku ya tukio, ndani ya ukumbi wa DEBORAH HALL pale Tel aviv, waziri mkuu, huku akiwa amevaa suti ya kiijivujivu, aliamua kutoa hotuba fupi ya dk 15, kwa kikosi hiki kilichokuwa kimekaa ukumbini hapo, askari hao waliokuwa wakiimba huku wameshikilia makopo ya bia za stella mikononi, tayari kusonga mbele.

Waziri mkuu alisema hivi "Makamanda wenzangu, ninalifahamu vizuri jeshi letu la REPUBLICAN GUARD, ninatambua kwamba mnao morali wa kutosha kuweza kushinda vita. Hili ni jeshi lenye historia ndefu kuliko jeshi lingine lolote duniani. Kama mnavyoona tunazo ndege aina ya B 53 bomber missile zenye uwezo wa kufika na kufanya mashambulizi popote duniani ndani ya dk 15. Lakini pia Idi Amin nimepata taarifa zake, kwamba anashirikiana na maaskari wa kiarabu! Waarabu nimepigana nao vita ya uchochoroni, Waarabu ninawajua.

Waarabu ni watu wanaotumia uzembe kidogo wa adui ili kusawazisha makosa. Makamanda wenzangu, huko muendako kuweni makini sana!! kuweni waangalifu chukueni tahadhali ya kutosha, wala msiruhusu uzembe wowote kutokea, iwapo mtaruhusu uzembe wowote kufanyika, basi wote kufumba na kufumbua mtafutika juu ya aridhi ya Uganda. "alimaliza hotuba yake waziri mkuu, huku akipigiwa makofi na askari hawa ambao walikuwa tayari kusonga mbele.

Maafisa wa Ubalozi wa Israel pale Nairobi Kenya, walikuwa wamepokea order toka Israel ya kumutafuta kwa gharama yoyote muafrika mwenye upeo wa kutosha lakini ambaye anafanana sana na Idi Amin kwa kimo, unene na sura. Basi maofisa hao walimpata na kumutuma Israel Mjaluo mmoja aliyeitwa Shakazulu. Ili aka act kama Idi Amin wakati watakapotua Entebe. Mjaluo huyo alipewa semina ya kutosha na mazoezi, alitakiwa pale airport aonekane kabisa kama Idi Amin na kuamuru mambo kadha wa kadha. Baada ya operesheni Mjaluo huyo alilipwa dau kubwa na kisha kupewa uraia wa Uingereza.

Baada ya hapo askari wote wa Kiyahudi waliingia kwenye SYNAGOGI moja la dini ya JUDAISIM ili kufanya ibada! Lakini pia nabii mmoja wa JUDAISIM alidai ile ndege ambayo ingewasafirisha ilipaswa kuongozwa na kijana mdogo kabisa ambaye hajakutana na mwanamke bado. Kijana wa kiume bikira!!

Hivyo alifwatwa kijana mmoja wa Kiyahudi mwenye umuri wa miaka 14 tuu, kutoka ktk chuo kidogo cha Hebrew pale Jerusalem aliyeitwa David. Kijana huyu ndiye aliyerusha ndege hiyo kubwa ya kijeshi yenye uwezo wa kubeba abiria 400. Na asikofu mmoja wa JUDAISIM alionekana akiwa amemuwekea mikono kichwani akimuombea.

Hayo yote yaliendelea kwa siri ya hali ya juu!! Ni taifa la Ufaransa tuu lililokuwa likijua siri hiyo! na mpaka leo hatujajua kwanini Wayahudi waliamua kumujulisha Mfaransa.

Dege liliambaa, inasemekana lilianza safari majira ya saa 4.15 jioni, inadaiwa dege hilo liliambaa usawa wa bahari ya shamu maarufu kama the red sea huku likiikwepa Cairo ya Gamal Abdunasser kisha likavuka Eritrea na kuingia Ethiopia baadae likaingia Kenya na lilipofika usawa wa Lake Victoria lilishuka chini sana usawa wa futi alfu nne tuu kutoka ktk njia yake ya kawaida ya futi alfu thelathini na tano angani, ili kuzikwepa rada za Entebe na Kampala.

Lakini inasemekana ktk anga la kimataifa usawa wa Entebe lilikuwepo dege jingine ambalo kwa vyovyote lisingeonekana kwa rada, nalo lilikuwa na jukumu moja tuu, kuangalia hali nzima ya usalama, kufuatilia maendeleo ya operesheni na kutoa msaada wa dharula kama ingelazimu kufanya hivyo!!
Ndani kabisa ya dege hilo, alikuwemo mwanasaikolojia mmoja wa Kiyahudi, aliyeitwa dk Shalmati, ambaye pia naye alikuwa askari na inadaiwa alikuwa amepitia chuo kimoja na Idi Amin, mwanasaikolojia huyu wakati ndege ikizidi kusogea mda wote alikuwa akiongea kwa njia ya simu na Amin kuhusu wale mateka, ili wakati mashambulizi yanaendelea simu ya Idi Amin iwe engaged hivyo asipate fursa ya kupokea simu nyingine, na alifaulu kumu keep busy!!
Itaendelea..................

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top