Je, ni nani aliyekuwa anaongoza ndege hiyo?? Maana rubani wa ndege shariti apate mawasiliano kutoka aridhini hasa kutoka kiwanja ambacho ndege itatua! Ndiyo maana rubani wa ndege hukaa amevaa airphone masikioni ili asipoteze mawasiliano. Akipoteza mawasiliano basi ndege inapotea!
Mpaka leo haijajulikana ni nani aliyekuwa akiongoza ndege hiyo hadi Entebe. Ila ndege hiyo ilipofika pale kisumu Kenya, iliwasiliana na maafisa wa anga wa Entebe, kwamba sisi ni marubani wa ndege moja ya kutoka muungano wa falme za kiarabu UAE, tulikuwa tunatoka Qutar tunaenda Durban South Africa, bahati mbaya tumepoteza mawasiliano, hivyo basi tunaomba tutumie kiwanja chenu cha Entebe kwa mda, ili tutafute tena mawasiliano, lakini pia tuchukue mapumuziko kwa mda. Waliruhusiwa kutua kwa mda Entebe.
Kamanda wa Kiyahudi wa jeshi hilo la ukombozi, alisimama ktk ya askari wake na kuanza kuimbisha nyimbo za kupandisha mzuka!! Mara wimbo huo ukadakwa na ndimi za askari hao 21 pamoja na wahudumu wengine wa ndege hiyo maarufu kama ma airhostess!!
Ndege hiyo ilipokaribia kiwanja hicho cha Entebe kama km 16 kabla, pale Entebe umeme ulikatika ghafla ktk mji wote wa Entebe na viunga vyake! pia mawasiliano yoyote ya redio na simu yalikatika mda huohuo! Nani aliyakata?? Mpaka leo haijajulikana ni nani aliyakata miundombinu hiyo. Vyanzo vingine vya habari vinasema, ciku mbili kabla tayari mashushushu wa Kiyahudi kutoka shirika la ujasusi la Israel (MOSWARD) walikuwa Entebe wakiwa wamevaa vilemba na makanzu kama waarabu huku wakijifanya kufanya booking za kusafiri, maana baada ya shambulio nao pia walitoweka na ndege hiyo.
Ndege ilianza kutua ikitumia mwanga mkali wa taa zake maalum!! Kufumba na kufumbua milango ilifunguka, na kitu cha kwanza kutoka kwenye ndege, lilitoka gari moja la kutembelea likiwa linafanana kama lilelile alilokuwa akitumia Idi Amin, Shakazulu naye alikuwa ndani ya gari hilo huku akiwa amepiga kombati kama zilezile za Idi Amin, wakati huo kamanda wa Kiyahudi Jonathan Netanyau mdogo wake Benjamini Netanyau alikuwa ameteremka chini siku nyingi!
Kisha yakatoka na magari mengine ya kijeshi yaliyokuwa yanafanana ambulance!! Jukwaa la Entebe la kuongozea ndege lilitekwa kwa mda na askari hawa wa kigeni. Mda huo wote hapakuwa na umeme wala mawasiliano yoyote. Shakazulu ndiye aliyeongoza msafara hadi pale kizuizini walikokuwa wamehifadhiwa mateka huku akitoa amri kadhaa kama Amin mwenyewe.
Ikumbukwe makomando hawa wa Kiyahudi usingewagundua mara moja!! Kwani usoni walikuwa wamevaa sura bandia zilzowafanya waonekane kama askari wa kiganda kabisaaa!! Bunduki zao zilikuwa na viwambo vya kuzuia sauti!! Hata magari yao yalifanana kabisa na yale ya jeshi la Uganda, hata platenumber zilionyesha namba za magari ya jeshi la Uganda!! Nani ambaye angegundua ujanja huo Katikati ya usiku wa giza la saa mbili unusu usiku??
Ujanja huo wa ki jasusi ulitosha kuwaaminisha askari walinzi wa korokoroni kwamba aliyekuwa akiongoza sekeseke hilo alikuwa ni Amini mwenyewe, hivyo kuanza kutii kwa haraka kila Shakazulu alichoamurisha. Hawakubomoa, mlango wa lockup ulifunguliwa na mlinzi wa zamu pale korokoroni, akitii amri ya Shakazulu aliyataka gereza lifunguliwe! Mle ndani mateka walikuwa wametengwa mara mbili, chumba kimoja mateka wa kiume na chumba cha pili mateka wa kike. Wakati makomando wa Kiyahudi wakifika gerezani hapo, Carlos aliyekuwa ni msimamizi mkuu alikuwa amekwenda haja ndogo, na hakurudi tena, je, Carlos alitowekaje maeneo ya gereza ambayo tayari yalikuwa yamezingirwa na makomando wa Kiyahudi???? Mpaka leo ni kitendawili hakuna anayejua Carlos alitowekaje!!
Makomando wa Kiyahudi walipoingia gerezani walikuta kwa ndani kumbe mateka walilindwa na maaskari wa Kipalesitina, Vijana wa Yasser Arafat toka chama cha HAMAS. Ndipo waliposema kwa lugha yao ya Kiyahudi (Rehibon bella llela) wakimaanisha wayahudi wote lala chini haraka sana, wale wote waliobakia wamesimama walikuwa ni waparestina na walipigwa risasi palepale, isipokuwa askari mmoja wa Kipalesitina alikuwa anaijua lugha ya Kiyahudi hivyo walipoamurisha Waisraeli kulala naye akalala chini, basi Vijana wa Kiyahudi walimugundua na wakamunyonga kwa mikono palepale chini.
Kamanda akauliza kwa lugha hiyo ya kwao, je, mko salama? je wenzenu wote wapo hapa. Huko nje magari yaliyokuwa Entebe yalikuwa tayari yote yametekwa!! Hakuna gari lolote lililoruhusiwa kutoka Entebe kwenda Kampala labda kutoka Kampala kuingia Entebe, kwa kweli usiku ule ilikuwa ni sekeseke na kifo kilikuwa njenje!!
Mwenzetu mmoja amepungua, walijibu mateka. Nani hayupo? Aliuliza kamanda, "Miss Bloach ndiye hayupo, homa imepanda akapelekwa Mlago hospital kutibiwa" alijibu mateka. Inasemekana walitaka wakamfate huyo bibi wa Kiyahudi lakini kamanda akapokea order kutoka makao makuu kule Tel aviv kwamba wamuache mda hautoshi.
Walikombolewa na mateka wengine wasiokuwa Wayahudi ktk operesheni hiyo. Mfano dk mmoja wa ki Marekani aliyekuwa amepigwa kisha kuwekwa ndani kwa kosa la kushukiwa kuwa na uhusiano wa ki mapenzi na mke wa Idi Amin bi Sarah!! Naye alitoroshwa na wasamaria wema gerezani na kisha kuambiwa, WAYAHUDI wapo wanakomboa wenzao pale Entebe na wewe nenda wakusafirishe, hapana hawatanielewa! Nenda bwana, wale ni wazungu wenzio watakuelewa tuu!! Alijibiwa na waliomutorosha. Mda huo wote Amin alikuwa akiongea kwa simu na mwana saikolojia wa Kiyahudi Dr Shalumat!!!
...... Itaendelea........
Post a Comment