................ Mwendelezo...............
Baada ya makomando wa Kiyahudi kuwafikia mateka, inasemekana kwanza waliwadunga sindano zenye kemikali ya mchanganyiko wa madawa ya kusisimua mwili, kuongeza nguvu na kujenga ujasiri! Kisha kwa haraka sana walivishwa kofia maalum vichwani zisizoruhusu risasi kupenya kwa urahisi na ngao za kukinga risasi vifuani na migongoni. Mwisho mateka wote 35 walikabidhiwa silaha aina ya shortgun, kumbuka kila Myahudi lazima apitie mgambo! Sasa mateka nao wakageuka askari na upele ukamfika mkunaji! Mpaka hapo zilikuwa zimekwenda dk nane tuu, Katikati ya operesheni siri ilivuja kwamba tayari Entebe imevamiwa na askari wasiojulikana. Viongozi wa ki serikali wa Entebe kwa mda waliangukiwa na mshangao wasijue wafanye nini.
Sasa mateka walikuwa wameanza kupakiwa ndani ya magari moja kwa moja mpaka kwenye ndege!! Mda huohuo askari wengine walikuwa wanafanya kazi ya kutoboa kwa risasi magurudumu ya magari yote yaliyokuwa airport pamoja na ndege. Vifaru vya kijeshi vya IDI AMINI vilivyokuwa uwanjani hapo vilikuwa tayari vimelipuliwa na rada zote zilifunguliwa vipandevipande. Ndani ya ndege mateka walizidi kuingizwa kwa kasi ya ajabu. Kamanda alipoiangalia saa yake, ikaonyesha bado dk mbili mda wa kutoka eneo la tukio kuisha. Kosa alilolifanya kamanda Jonathan Netanyau ni kuvua masiki yake ya chuma iliyokuwa kichwani ili kuipachika radio call yake vizuri na kupiga makao makuu kwamba operesheni tayari imekamilika. Askari mmoja wa Idi Amin aliyeitwa Basaja Balaba alikuwa amepigwa risasi akazirai, wao walidhani amekufa, basi askari huyo alijikokota kikomandoo na kuushika mgobori mmoja uliokuwa hapo na kisha kumulenga na kumufyatua kichwani kamanda Jonathan Netanyau, risasi ile ilimurusha juu kisha akaangukia kifua! Alisema maneno mawili tuu, "SITAFIKA ASUBUHI" "akakata roho!!! Ukawa ndiyo mwisho wa Jonathan Netanyau mdogo wake Benjamini Netanyau waziri mkuu wa sasa wa Israel!!
Makamanda wenzake walimumalizia kwa risasi askari huyu wa kiganda aliyemuua Netanyau!! Kisha askari huyo aliyemuua kamanda, maiti yake waliisafirisha hadi Israel ili wakaipime ubongo kuangalia hivi huyu jamaa aliyemuua kamanda alikuwa na TIMING kiasi gani!!
Taarifa ziliweza kumfikia mkuu wa nchi kwamba Entebe kumevamiwa, na Amin alianza kutoa amri vikosi vyake kuelekea Entebe haraka sana!! Dege lilifunga milango na kuanza kuondoka, matairi ya dege hili yakakamata lami ya uwanja huu wa Entebe nayo lami ikazitii. Ktk uwanja wa Entebe wayahudi waliacha wametegeshea Vifaru vilivyokuwa vinatema risasi utadhani ndani kuna askari. Sasa dege lilianza kuchana anga huku likitema mawingu mazitomazito ya moshi mweusi tii. , huku dege likitema mafataki yaliyofyatuliwa na kuacha sura za miti ya minazi angani.
Ndani ya ndege na Israel kwenyewe tarumbeta na vinanda vilipigwa mfululizo pasipo kukoma!! Makomando hawa hawakujua ni nini kilichokuwa kinawasubiri kule nyumbani. Hakuna lugha yoyote ya ki binadamu inayoweza kuelezea shamrashamra na furaha waliyoikuta pale nyumbani. Wayahudi wengi akili zili stuck huku wakijiuliza hivi ni kweli ama tunaota??
Wapo waliozirai!! Vijana wa kihuni na wasela wa Kiyahudi walilala wanashangilia na kutembea usiku kucha, wahuni walikuwa wanatoa vitu madukani pasipo kulipa, serikali ilisema wasishitakiwe ni furaha tuu!! Bar zilinywesha watu mpaka chwee!!
Kule Uganda mtangazaji mmoja wa redio kutoka kabila la Acholi, akajisahau na kutangaza kwa lugha ya kikwao kama ifuatavyo, (abayuda babatwalide Idi Amin talikumana) akimanisha Wayahudi wamechukuliwa na Idi Amin hajui!! Amin kusikia hilo tangazo akaja juu!! "yahaani wayahudi wamechukuliwa na mimi sina habari??? Basi hilo kabila Amin alikuwa amelipiga marufuku mtu yeyote wa kabila hilo kusomea uandishi wa habari.
Idi Amin hasira zilizomtoa hapo!! alimufuata mlango hospital mateka wa Kiyahudi bi Bloach na kumunyongelea mbali!! ila maiti yake baadae wayahudi walikuja wakaichukua na kuizika kule kwao.
Kiwanja kimoja cha ndege pale Tel aviv Israel kimeitwa kwa heshima ya jina la Netanyau, yahaani kunaitwa, CAPTAIN JONATHAN NETANYAU INTERNATIONAL AIRPORT.
simulizi yetu nzuri ya masaa 24 hapo ndipo inapofikia mwisho. Tunawashukuru wadau wote wa group hili. Kumbukeni tumepata hii story kwa hisani ya mama Kaengesa. Kumbukeni kumwambia asante kwa kumchangia. Muda wa kande sasa, mwenye blueband sawa, mafuta ya nguruwe ok, maharage poa.
Post a Comment